Legal Update – 20 Machi 2020

Tume ya Ushindani Yachukua Hatua Kulinda Walaji Katika Kipindi Hiki cha Mlipuko wa Corona

  • Tume ya Ushindani Tanzania imewaonya waagizaji, wafanyabiashara, wazalishaji, wasambazaji wa dawa za kutakasa mikono na maeneo yanayoweza kuguswa kwa mikono, barakoa na vizuizi vya mikono/glovu
  • Uchunguzi wa awali unaonyesha bei ya bidhaa hizo kupanda maradufu baada ya mlipuko wa corona
  • Kupanga bei baina ya washindani, kuficha, kupunguza, au kukataa kusambaza sokoni bidhaa kwa lengo la kupandisha bei na kujipatia faida kubwa isivyo halali, na vitendo hadaifu dhidi ya walaji wa bidhaa kuhusiana na uhalisia na usahihi wa aina ya bidhaa

Tume ya Ushindani Tanzania inakuwa moja kati ya mamlaka chache Barani Afrika kuonya waagizaji, wafanyabiashara, wazalishaji, wasambazaji wa dawa za kutakasa mikono na maeneo yanayoweza kuguswa kwa mikono, barakoa na glovu kuwa kujipangia bei, kuficha, kusababisha uhaba, kukataa kuuza bidhaa husika wakati wa janga la corona ni kosa chini ya Sheria ya Ushindani ya 2003.

Mnamo tarehe 19 Machi 2020, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dk. John Mduma alionya kwamba kumekuwa na malalamiko juu ya uhaba na upandishwaji bei kinyemela wa bidhaa husika. Onyo linasomeka, “Tume ya Ushindani imechunguza na kubaini kuwa malalamiko hayo ni ya kweli, inawakumbusha waagizaji, wafanyabiashara, wazalishaji na wasambazaji kwamba Tume ya Ushindani inakataza udanganyifu katika biashara kama vile kupandisha bei kiholela, na mengineyo,”

Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ushindani inabainisha kwamba:

9.- (1) Ni marufuku mtu yoyote kufanya au kutekeleza makubaliano ambayo lengo lake au matokeo yake ni: (a) kupanga bei kati ya washindani; (b) washindani kula njama ya kukataa kusambaza bidhaa; au (c) kula njama katika kuomba zabuni au ugavi. (2) Katika kifungu hiki:
(a) “kula njama ya kukaa kusambaza bidhaa baina ya washindani’’ kuna maanisha kupanga, kuzuia au kudhibiti bei, ushuru au tozo zingine kwa, au vigezo au masharti ambayo, muhusika katika makubaliano atasambaza au kupata, au kuomba kusambaza au kupata, bidhaa au huduma, katika ushindani na muhusika mwingine yeyote katika makubaliano;
(b) “washindani kula njama ya kukataa kusambaza bidhaa” inamaanisha:
(i) kuzuia muhusika katika makubaliano kusambaza bidhaa au huduma kwa watu fulani, au kununua bidhaa au huduma kutoka kwa watu fulani, katika ushindani na muhusika mwingine yeyote kwenye makubaliano;
(c) ‘’vizuizi vya pato kati ya washindani ‘’ maana yake ni kuzuia, kukwaza au kudhibiti uzalishaji wa muhusika mmoja katika makubaliano ya bidhaa au huduma zinazotolewa, katika ushindani na muhusika mwingine yeyote kwenye makubaliano;

Chini ya Sheria ya Ushindani, makosa yaliyotajwa hapo juu yanaweza kusababisha kutolewa kwa maagizo ya kufuata utaratibu na au adhabu kali hutolewa, hadi asilimia 10 ya mapato ya mkosaji. Adhabu kama hizo zinaweza kutolewa kwa kipindi cha miaka 6 kutoka tarehe ya kosa husika na uzoefu unaonyesha kuwa Tume ya Ushindani haiogopi kuchukua hatua kali.

Hatua hii ya Tume ya Ushindani ni muhimu katika kipindi hiki ambacho walaji wanapambana na athari za virusi vya corona.

Katika taarifa yake, Tume ya Ushindani imetoa namba ya simu kwa ajili ya kupiga na kutoa taarifa ili kupambana na tabia inayozuia ushindani wa kibiashara.

Watumiaji wanaweza kupiga simu ya bure kwa namba ifuatayo: Simu: 0800110094 au barua pepe: info@competition.or.tz

Kusoma toleo la Kiswahili la Ilani ya Tume ya Ushindani bonyeza hapa.